
Dar es Salaam: Habari ya mjini kwa sasa ni ujauzito wa Wema Isaac
Sepetu ambapo inadaiwa kuwa ameanza mazoezi ya kumlea mtoto wake
mtarajiwa.
Kwa mujibu wa shosti wake wa karibu, kwa sasa Wema
ameongeza urafiki kwa akina mama wenye watoto wachanga ili kuchukua
‘maujuzi’ ya namna ya kuwa mama bora kwa mwanaye mtarajiwa.
“Yaani
ukitaka kujua Madam yupo bize na mazoezi ya kulea, kila tunapokwenda
akimuona mama aliyemzoea mwenye mtoto basi ataomba ambebe mtoto acheze
naye au hata amlishe.
“Kweli Wema anapenda watoto lakini sasa hivi
imekuwa too much (imepitiliza). Hata ukifuatilia kwenye akaunti zake
kwenye mitandao ya kijamii utaona sasa hivi yupo bize kutupia picha
akiwa amebeba watoto,” alisema shosti huyo wa karibu wa Wema na
kuongeza:
“Kiukweli bidada (Wema) yupo kwenye mazoezi makali ili
awe mama bora kwa mwanaye mtarajiwa kwani alitamani kuwa na mtoto kwa
muda mrefu.”
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, gazeti lilimtafuta
Wema ili kujua anaendeleaje na mazoezi ya kulea mwanaye mtarajiwa lakini
simu yake iliita bila kupokelewa.

0 comments:
Post a Comment