STAA asiyeishiwa vituko Bongo, Wema Sepetu juzikati aligonga tena
vichwa vya habari baada ya kukataa kula keki ya sherehe ya kumbukumbu ya
siku ya kuzaliwa ya rafiki yake aliyefahamika kwa jina la Chidy
Mapenzi, kwa kile kilichodaiwa kuwa hakualikwa.
Chanzo chetu cha kuaminika kinadai kuwa wakiwa katika mitoko yao ya
kila siku, Wema, Aunt Ezekiel na Kajala walijikuta wameibukia Club
Billicanas kwa ajili ya kujirusha. Wakiwa ukumbini hapo, ghafla muziki
ulizimwa na tangazo kutolewa kuwa siku hiyo, Chidy Mapenzi alikuwa
anasherehekea siku yake ya kuzaliwa yaani bethidei.
Baada ya tangazo hilo, Chidy alipanda jukwaani na baadhi ya marafiki
zake wakaitwa ili kula keki iliyoandaliwa, lakini alipoitwa Wema,
alikataa kwa madai ya kutoalikwa rasmi katika shughuli hiyo.
“Watu walimshangaa sana Madam, alipoitwa akakataa katakata, na hata
Kajala naye alipoitwa alienda lakini akakataa kula keki, akaibeba na
kumpelekea Wema aile, bado akakataa,” kilisema chanzo hicho.

0 comments:
Post a Comment