Tuesday, January 5, 2016

Saudia
Ubalozi wa Saudi Arabia mjini Tehran ulichomwa na waandamanaji


Baraza la Usalama la UN, likijibu barua kutoka kwa Saudi Arabia, limeshutumu shambulio hilo la katika ubalozi Tehran pamoja na shambulio katika afisi ya ubalozi wa Saudia Arabia katika jiji jingine la Iran la Mashhad...,


 
Baraza hilo limeitaka Iran kulinda mabalozi na mali ya ubalozi pamoja na wafanyakazi wake “kwa mujibu wa makubaliano ya kimataifa”.
Limetoa wito kwa pande zote mbili “kushauriana na kuchukua hatua za kupunguza wasiwasi katika kanda hiyo”.

Hata hivyo, baraza hilo halijazungumzia hatua ya Saudi Arabia kumuua Sheikh Nimr al-Nimr, mhubiri wa madhehebu ya Shia, aliyeuawa Jumamosi pamoja na watu wengine 46 baada ya kutuhumiwa kutekeleza makosa yanayohusiana na ugaidi.
Iran
Maandamano Makubwa Nchini Iran ya Kuipinga Saudi Arabia
 
Akizungumza New York, balozi wa Saudi Arabia katika UN Abdallah al-Mouallimi amesema mzozo wa sasa ungeepukika iwapo Iran ingejiacha

 “kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine, ikiwemo Saudi Arabia”.

Awali, Saudi Arabia imewahi kuituhumu Iran kwa kuingilia masuala ya ndani ya nchi za Kiarabu.
Saudi Arabia na Iran ndizo nchi kuu za Kisuni na Kishia mtawalia eneo la Mashariki ya Kati na zimekuwa wapinzani wakuu.

Nchi hizo huunga mkono pande pinzani katika mizozo Syria na Yemen.
Nimr
Hukumu ya Kifo cha Shekh Sheikh al-Nimr ilitekelezwa jumamosi

 

Bw. Mouallimi amesema juhudi za kutafuta Amani katika mataifa hayo hazifai kuathiriwa na mzozo wa sasa.

Kufuatia mashambulio hayo, nchi kadha washirika wa Saudi Arabia zimekatiza uhusiano na Iran zikiwemo Bahrain na Sudan na Jumuiya ya Milki za Kiarabu (UAE) ambayo imepunguza hadhi ya ujumbe wa kibalozi wa Iran.

Somalia pia imesema inaunga mkono hatua ya Saudi Arabia kuvunja uhusiano na Iran.

0 comments:

Post a Comment