Kamanda
wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Operasheni
kali inayoendelea jijini Dar es Salaam
Na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
WAMILIKI
wa Taasisi za Kifedha wanatakiwa kujiridhisha kama waajiliwa katika
taasisi hizo kama wanahusika kwa njia moja ama nyingine katika uharifu
unaohatarisha maisha ya wakazi wa jijini la Dar es Salaam.
Hayo
yamesemwa na Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon
Sirro wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za makao
makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam leo.
Kamanda Sirro amesema kuwa hatua za makusudi zimechukuliwa katika maeneo mbalimbali hasa ya eneo la Kibiashara la Mlimani City kutokana na matukio mengi ya uporaji wa fedha kwa kutumia pikipiki.
Pia
amesema kuwa pamoja na sheria hizo kuchukuliwa watafanya operasheni
maalumu katika eneo hilo na kutafuta namna nzuri ya kuondoa pikipiki
katika maeneo hayo.
Katika
Operasheni zilizofanywa na Jeshi hilo wamefanikiwa kuwakamata majambazi
nane pamoja na kumamata Bunduki mbili aina ya Pump Action ambazo namba
zake zilifutwa na kukatwa Mtutu.
Aidha
Kamanda Sirro amesema kuwa katika Operasheni hiyo wamemkamata jambazi
aliyekuwa akitafutwa kwa muda mrefu anayejulikana kama Mkama Hassan
mkazi wa Gomgolamboto jijini Dar es Salaam na alipopekuliwa alikutwa na
Bastola aina ya Chinese iliyofutwa
.
Kamanda wa Polisi kanda maalumu
ya Dar es Salaam, Simon Sirro akionyesha Siraha zilizokamatwa katika
Oparasheni ya kutokomeza uharifu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari
wakimsikiliza Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon
Sirro leo wakati akizungumuza nao
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.




0 comments:
Post a Comment