·
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Masauni.
Ziara yangu ya kikazi katika Makao Makuu ya Uhamiaji, Nimetoa maagizo yafuatayo;
1. Operesheni maalum ifanywe na Uhamiaji kuyapitia makampuni yote yanoajiri wageni na kuwabaini raia wote wa kigeni wanoishi nchini kinyume na sheria ikiwemo wanaofanya kazi zinazoweza kufanywa na Watanzania na kuziba fursa za mamia ya vijana wa kitanzania wanaohangaika kutafuta kazi, wafanya kazi tofauti na vibali vya kazi walizomba, wanaojishuhulisha na shughuli za siasa na uhalifu ikiwemo kuwanyanyasa na kuwadhalilisha wananchi, kukwepa kulipa kodi na uharamia wa aina mbali mbali na kuwaondosha nchini mara moja. Tarifa ya awali ya utekelezaji wa agizo hilo iwasilishwe ofisini kwangu baada ya siku 7.
Pili. Nimeagiza uchunguzi wa kina ufanyike ili kuwabaini wahusika walotumia vibaya utaratibu wa utoaji vibali vya ukaazi vya muda (CTA), kwa kuwapatia wasiohusika, kuvitoa kiholela na kushindwa kufuatilia mpaka kupelekea kufutwa kwa vibali hivyo, na kuathiri mapato pamoja na kusababisha usumbufu kwa wageni wanaokuja nchini kwa shuhuli muhimu za muda mfupi na kuwachukulia hatua watumishi hao ambao si waaminifu ili utaratibu mpya unaoandaliwa uweze kuleta ufanisi.
3. Nimeagiza mchakato wa kuanzisha Mahakama ya kijeshi uharakishwe ili wezi na wala rushwa waweze kushuhulikiwa kwa haraka.


Duh, sasa nchi imeamka maana kila kukicha mambo yanalipuka, yaani ni kwamba watu walipewa fursa wao wakatumia vibaya wananvyotaka wao mpaka kuwa Miungu watu, ona sasa kila kona kuna wageni na kila mara unapotoa taarifa katika vyombo husika unakuta hakuna anayefuatilia zaidi ni wale waliopewa nafasi kujinufaisha wao na kuachia wageni kufanya wanavyotaka. Hii ni hatari napendekeza hiyo Mahakama ya Kijeshi ianzishwe haraka kuwashughulikia hawa watu na nafikiri wahusika wote wakijulikana na kukamatwa dawa si kuwafunga ni kuwaua hata kama taasisi za haki za binadamu zitalalamika wacha zilalamike wametuharibia nchi yetu hawa washenzi.
ReplyDelete