Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika kazi ya kujenga msingi wa chumba cha maabara katika shule ya sekondari kata ya Unyanga Singida ikiwa ni shuguhuli za maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM yanayotarajiwa kufanyika mjini Singida Jumamosi Februari 6 mwaka huu kwenye uwanja wa michezo wa Namfua mkoani humo, Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “Kufanya Kazi” (PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-SINGIDA)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikiana na mafundi katika ujenzi wa msingi chumba cha maabara sekondari ya kata ya Unyanga Singida tayari kwa maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM yanayotarajiwa kufanyika mjini Singida Jumamosi Februari 6 mwaka huu kwenye uwanja wa michezo wa Namfua mkoani humo.
Baadhi ya wananchi wakiendelea na akzi ya kuchanganya mchanga na sementi kwa ajili ya ujenzi wa maabara hiyo.
Baadhi ya mafundi wakiendelea na kazi yao katika ujenzi huo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisshiriki katika kazi ya kupalilia shamba kwa kutumia mifugo yaani Ng’ombe na jembe la Plau katika shamba la mtama la mkulima Elisha Abdalla lenye ukubwa wa ekari moja na nusu katika kata ya Mtamaa wilayani Singida Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Kufanya Kazi”
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiendelea na kazi katika shamba hilo.Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Kufanya Kazi”
Mkulima Bw . Elisha Abdalla akimuelezea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana jinsi anavyolima shamba lake kisasa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi mara baada ya kushiriki kazi ya kupalilia shamba la mtama la Bw. Elisha Abdalla wa kata ya Mtamaa wilayani Singida.
Baadhi ya wajasiriamali wa wilaya ya Singida wanaojishghulisha na biashara ya Mama Ntilie, Bodaboda na matunda wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katika mkutano uliofanyika kwenye ofisi ya CCM mkoa wa Singida.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajasirialmali wa mjini Singida wakati alipokutana nao kwenye ofisi ya CCM mkoa wa Singida na kusikiliza matatizo yao ili kuyapatia ufumbuzi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Afisa biashara wa Manispaa ya SingidaBwErick Sinkwembe wakati alipokutana na wajasiriamali kwenye ofisi ya CCM mkoa wa Singida na kusikiliza matatizo yao ili kuyapatia ufumbuzi.
0 comments:
Post a Comment