Dar es Salaam. Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman amesema suala la uanzishwaji wa Mahakama maalumu ya kushughulikia makosa makubwa ya ufisadi, rushwa na uhujumu uchumi ndicho kipaumbele kikuu na cha kwanza kwa mhimili huo wa dola mwaka huu.
Jaji Mkuu alisema hayo jana alipozungumza na mwandishi wa Mwananchi kuhusu mchakato wa uanzishwaji wa mahakama hiyo ambao unatokana na ahadi ya Rais John Magufuli aliyoitoa wakati wa kampeni zake katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, ikiwa ni hatua ya kukabiliana na vitendo vya ufisadi.
Novemba mwaka jana, Jaji Kiongozi, Shaban Lila alikaririwa na gazeti hili akisema tayari mchakato wa uanzishwaji wa mahakama hiyo umeshaanza kwa wadau wa haki jinai kujadili iwapo ianzishwe kama kitengo ndani ya Mahakama Kuu au iwe Mahakama huru.

0 comments:
Post a Comment