Hajji Khamis
Jumuiya
ya Watanzania New York, New Jersey na Pennsylvania (NYTC) imepokea
habari za msiba ambazo zimethibitishwa na kuruhusiwa kutangazwa na ndugu
Michael Chiume kwa niaba ya familia ya Chiume. Dada yetu mpendwa Jessie
Chiume hatunaye duniani. Amefariki leo asubuhi kwa kugongwa na gari
huko Mount Vernon, NY. Mungu ailaze roho ya dada yetu Jessie mahali
pema peponi. Ni wakati mgumu sana kwa familia ya Chiume na sisi wote
Watanzania ndugu zake. Habari zaidi za mipango zitatangazwa na jumuiya
au familia ya Chiume kadri zitakavyopatikana.
RIP Jessica Chiume. We love you, we will miss you.


0 comments:
Post a Comment