Imeelezwa kuwa Mashaka, ambaye pia ni ofisa intelijensia wa hifadhi hiyo, anadaiwa kuwa kinara mkubwa wa ujangili katika hifadhi mbalimbali zilizoko Kanda ya Ziwa kwa kutoa ushirikiano kwa majangili pamoja na kuwaazimisha silaha za kufanyia uhalifu huo.
Hii ni aibu sana, wale tunaowaamini ndio wanaotuangusha. Nashauri sheria za hifadhi za taifa zifanyiwe masahihisho ili watu kama hawa wanyongwe na kufilisiwa mali zote.
Nchi hii imeoza kila sehemu sasa kama huyu msimamiaji mwenyewe ndio jangili mwenyewe mkuu."
Mhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, Iddi Mashaka,
amekamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuhusika na tukio la utunguaji wa helikopta namba 88HF na kusababisha kifo cha rubani wake, Rogers Gower, raia wa Uingereza.
Ilielezwa kuwa Mashaka, ambaye pia ni ofisa intelijensia wa hifadhi hiyo,
anadaiwakuwa kinara mkubwa wa ujangili katika hifadhi mbalimbali zilizoko Kanda ya Ziwa kwa kutoa ushirikiano kwa majangili pamoja na kuwaazimisha silaha za kufanyia uhalifu huo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Lazaro Mambosasa, alisema Mashaka (49) ni mwajiriwa wa Hifadhi ya Ngorongoro.
Kamanda Mambosasa alisema Jeshi la Polisi mkoani Simiyu, chinio ya Mkuu wa Upelelezi, Jonathan Shana, liliendesha msako maalumu uliowashirikisha askari wa vyeo mbalimbali, kikosi kazi na askari wa wanyamapori na wananchi, hivyo kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wenzake wanane walioshiriki katika tukio hilo.
Kamanda aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Shija Mjika, Njile Gonga, Masasi Mandago, Mwigulu Kanga, Mapolu Njile, Dotto Huya, Mange Balum na Dotto Pangali
ambao walidaiwa kuhusika na tukio hilo la kikatili lililokatisha maisha ya rubani wa helikopta iliyokuwa ikifanya doria eneo la Gululu ndani ya Hifadhi ya Maswa katika kitalu cha mwekezaji, Mwiba Holding Ltd.
Alimtaja Dotto Pangali kuwa ndiye aliyetungua ndege hiyo kwa kutumia bunduki aina ya Rifle namba 7209460 CAR na 63229 na kwamba alipohojiwa alikiri bunduki hiyo ni mali ya Mange Magima. Kamanda Mambosasa alisema katika tukio hilo, Shija, Njile na Masasi Mandago, walitoa ushirikiano wa karibu kwa kuwaonyesha meno mawili ya tembo yenye uzito wa kilo 31 waliyokuwa wameyaficha chini ya daraja katika kijiji cha Itaba.
#SasaKaziTu
Source: Polisi Tanzania

Allen Kicharungu

0 comments:
Post a Comment