![]() |
|
Kuanzia jana jioni,
habari zilienea kwenye mitandao ya kijamii na hasa Twitter kwamba
mlanguzi hatari wa dawa za kulevya Joaquin Guzman, maarufu kama EL Chapo
alikuwa ametoroka jela tena.
Je, zilikuwa za kweli?La hasha. Habari hizi zilitokana na tovuti ya habari za kubuni ya abcnews.com.co ambayo imefanywa kuonekana kana kwamba ni ya shirika tajika la habari la Marekani la ABC News ambalo tovuti yake halisi ni abcnews.go.com. Habari hizo za kubuni, zilieleza jinsi walinzi wawili wa gereza walivyoonekana wakiwa wamemshika El Chapo, kana kwamba wanamhamisha kutoka seli moja hadi nyingine, mwendo wa saa nane usiku na baadaye ikadaiwa kwamba ametoweka pamoja na walinzi hao. Wengi waliamini habari hizo na wakaanza kujadili kutoroka kwake jela kana kwamba ni tukio lililokuwa limefanyika. Hilo lilifanya jina lake kuvuma sana katika mitandao ya kijamii. Baadhi walisema iwapo El Chapo alikuwa amefanikiwa kutoroka jela mara ya tatu, basi hata akienda jehanamu atafanikiwa kutoroka. Alikamatwa tarehe 8 Januari baada ya kuwa mtoro kwa zaidi ya miezi sita. Kwa sasa, utaratibu wa kumhamishia Marekani akajibu mashtaka unaendelea. El Chapo alikuwa ametafutwa sana baada ya kutoroka jela tarehe 11 Julai mwaka 2015, akipitia shimo lililochimbwa chini ya gereza hadi kufikia seli yake gerezani. Marekani ilikuwa imeahidi zawadi ya $5m kwa mtu ambaye angetoa habari za kuwezesha kukamatwa kwake. Alikaa mafichoni mwa miaka 13 kabla ya kukamatwa na kufungiwa Altiplano mwaka 2014. Tovuti hiyo bandia imewahi kutoa habari za uongo awali ambazo watu walizisambaza na kudhani ni za kweli. Mfano ni habari kwamba Rais Obama alikuwa ameidhinisha sheria ya kuwataka watu wanaomiliki silaha wawe wakiruhusiwa kumiliki bunduki tatu pekee. Wakati mmoja, walitangaza pia kwamba Donald Trump alikuwa amemtangaza Sheriff Joe Arpaio kuwa mgombea mwenza wake. |
Monday, February 1, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


0 comments:
Post a Comment