Tuesday, February 16, 2016

kig2
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akimwangalia mtoto aliyeugua ugonjwa wa kipindupidu  katika kituo cha afya cha Mtakatifu Lucas (Kambi ya ugonjwa huo) kwenye  eneo la Mboliboli kutokana na marufiko yaliyotokea katika kijiji cha Idodi, Iringa ambayo yalisomba nyumba na vyoo baada ya mto Ruaha kujaa maji kubadilisha mkondo wake.

kig3
Baadhi ya wagonjwa wakiendelea kunywa maji maalum kwa ajili ya kuongeza nguvu baada ya kukumbwa na ugonjwa  huo katika kambi maalum ya ugonjwa huo   iliyopo katika kituo cha afya cha Mtakatifu Lucas.kwenye wilaya ya Iringa Mjini.
kig4
Baadhi ya        maeneo yaliyokumbwa na marufiko katika eneo la mashamba ya mbunga lijulikalo kwa jina la Nyalu
kig5kig6
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akifyeka majani kwa ajili ya njia kuelea eneo lilikubwana mafuriko katika eneo la mashamba ya mbunga Nyalu.
kig7
Rubani wa ndege ya Jeshi la Polisi, Flora Focas akimwokoa mama mjamzito na kumuingiza katika chopa iliyompeleka Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye aliamuru chopa hiyo imchuke mama huyo ili kuokoa miasha yake.
kig8
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla  akitokea kwenye eneo la pori kwenye  mashamba ya mpunga ya Nyalu kwa ajili ya kuangalia watu waliozingirwa na maji ili wawezekuokolewa . Alikuwa amembatana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini, Richard Kasesela.
kig9
Akina mama wenye watoto wadogo mtoto wa wiki moja na  miezi miwili wakiondolewa  katika eneo la marufiko katika mashamba ya Nyalu  wilaya  ya Iringa .
Picha  zote na MAGRETH KINABO -MAELEZO

0 comments:

Post a Comment