
Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop, Dudu Baya amedai kuwa alikabidhiwa rapa Dogo Hamidu ‘Nyandu Tuzi’ na Mama wa msanii huyo ili amlee.
Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Dudu Baya amesema anajivunia mafanikio ya msanii huyo, kwani kwake ni kama mtoto wake.
“Unajua hata mama yake Nyandu alivyofariki aliniambia nakuachia mwanangu, nilelee mtoto wangu, na Nyandu hakuwahi kumjua baba yake, so nikawa namlea Nyandu kama mwanangu, nikamwambia dogo sikupeleki studio mpaka usome kwanza. Ndio akaenda shule, ila kwa sasa najivunia mafanikio yake kwani ni sawa na mtoto wangu mwenyewe”, alisema Dudu Baya.
Kuhusu kipigo alichowahi kumpa Nyandu Tozi baada ya kuacha chenji ya sh. 300 dukani, Dudu baya alisema alimpiga ili kumfundisha juu ya matumizi ya hela, na si vinginevyo kama watu wanavyofikiri
0 comments:
Post a Comment