Sunday, February 14, 2016

madee
Msanii wa bongo fleva kutoka tip top connection Madee amesema mahudhurio yake kwenye viwanja vya burudani yamekuwa mabovu kutokana na ukweli kuwa ametingwa na malezi ya mwanae wa kike ambaye kwa sasa yuko likizo.

Pia Madee ameweka wazi kuwa hata muda huu hajaachia kazi yoyote kutokana na sababu hiyo na kuongeza kuwa inabibi akabe nafasi ya ubaba na umama kwa kuwa haishi pamoja na mama wa mtoto huyo.
Mimi siwezi kwenda club kila siku kwa sababu nina mtoto nalea kwa hiyo inatakiwa niwe makini nae,nalala mapema naamka mapema ili nijue anaishi vipi..hata ngoma nimeacha kutoa mpaka atapoenda shule” alifunguka Madee ambaye alidai kwa mwaka mzima anakaa na mwanae miezi miwili tu ,miezi mingine yote anakuwa shule.
Source:Clouds Fm

0 comments:

Post a Comment