Posted by Williammalecela.com on Sunday, February 07, 2016
Maswali mengi yameibuka hivi karibuni
baada ya wadau mbalimbali wa masuala ya siasa kutolisikia jina la mbunge
wa kigoma mjini Zitto Kabwe kwa tiketi ya ACT Wazalendo likitajwa na
mwenyekiti wa kambi rasmi ya upinzani bungeni Freeman Mbowe katika
baraza la mawaziri vivuli.
Kiongozi wa Kambi rasmi ya upinzani
Bungeni, Freeman Mbowe jana alitangaza orodha ya majina ya wabunge wa
upinzani wanaounda baraza la mawaziri vivuli, huku akimtosa Mbunge wa
Kigoma Mjini, Zitto Kabwe.
Maswali mengi yaliibuka na kuzua mjadala
kwanini Mbowe ameamua kumuacha Zitto haliyakuwa hivi karibuni
wameshirikiana vyema katika kupinga hoja za serikali ikiwemo ile ya
kutooneshwa LIVE kwa vipindi vya Bunge katika luninga ya Taifa TBC, na
kutoka na tamko moja kama wapinzani.
“Ukawa tulisaini tamko la pamoja la
ushirikiano na hiyo ilikuwa katika Bunge la Katiba. Kumbuka
tumeshirikiana katika Uchaguzi Mkuu na kupata madiwani na wabunge ambao
ndiyo hawa wamezaa baraza hili,”
“Ushirikiano wetu upo katika halmashauri
na majiji. Kutokana na jambo hilo huwezi kuiingiza ACT maana haikuwapo
katika makubaliano ya Ukawa,”
0 comments:
Post a Comment