Ujanja wa mjini! Jamaa aliyejipachika cheo kuwa yeye ni Afisa Usalama wa Taifa, Ofisi ya Waziri Mkuu akijitambulisha kwa jina moja la Manase amekiona cha moto baada ya kunaswa na kufungwa kamba mwilini na mtu aliyesema ni daktari wa Kliniki ya Head 2 ya jijini Dar, Fortdas Fidell.
Tukio hilo la aina yake lilitokea Jumatano ya Februari 10, mwaka huu katika kliniki hiyo inayojishughulisha na tiba ya mifupa na mazoezi iliyopo Mtaa wa Ununio, Kata ya Kunduchi wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo risasi sita zilipigwa hewani na mtu aitwaye Mashaka Ndonde ili kumdhibiti mtuhumiwa huyo.
0 comments:
Post a Comment