Mwenyekiti
wa CCM taifa, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,ametangaza rasmi kwamba
sherehe za maadhimisho ya CCM kutimiza miaka 39 toka kianzishwe
zinazofanyika kitaifa leo Singida zitakuwa za mwisho kwake kuwa
mwenyekiti wa chama hicho kikongwe nchini.
Bila kutoa ufafanuzi
zaidi,Dkt. Kikwete ambaye alikuwa ameongozana na mke wake mama Salma,
alisema anafuraha mno kuwa alianza kazi ya kuitumikia CCM kwa mara ya
kwanza hapa mjini Singida Aprili 1975,na anamalizia Singida mjini
Februari sita mwaka huu.
Dkt. Kikwete ambaye ni rais
mstaafu wa awamu ya nne,aliyasema hayo jana jioni wakati akizungumza na
baraza la wazee la Manispaa ya Singida kwenye ukumbi wa mikutano wa
kanisa katoliki mjini hapa.
Aidha,mwenyekiti huyo
alilishukuru baraza la wazee Manisaa ya Singida kwa juhudi zao
kukisaidia Chama Cha Mapinduzi kupata ushindi mnono katika uchaguzi mkuu
uliopita.
“Mkutano mkuu uliopita, ulijaa
changamoto nyingi na kwa kifupi,ulikuwa mgumu mno.Bila busara zenu
ninyi wazee,kwa sasa pengine tugekuwa tunazungumza hadithi nyingine,
mmefanya kazi kubwa,msichoke endeleeni kukitetea chama chenu ili amani
na utulivu uendelee kudumishwa,” alisema.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa
miaka yote mkoa wa Singida umeendelea kuwa ngome imara ya CCM, kwa hali
hiyo,amelitaka baraza la wazee wasiache sifa hiyo ikapotea.
Kwa upande wa serikali ya Dkt.Magufuli, alisema yeye anaiunga mkono na kuitakia kila la kheri katika kuwatumikia wananchi.
“Niwaombe na ninyi wazee na
wakazi wote wa mkoa wa Singida, muiunge mkono serikali hii ya awamu ya
tano imeonyesha dalili nzuri katika kutekeleza majukumu yake mkiacha
kuiunga mkono, mtaikatisha tamaa kwa hali hiyo, itashindwa kuwatumikia
wananchi ipasavyo,” alisema Dk.Kikwete.
Wakati huo huo, serikali ya rais Dk.Magufuli inatajiwa kuhamia Singida
mjini kwa siku nzima ya leo kushiiki sheehe za maadhimisho ya kitaifa
CCM kutimiza miaka 39 toka kianzishwe.
Kwenye sheehe hizo ,akamu wa
Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Wazii Mkuu Mhe. Majaliwa Kasimu
Majaliwa, mawaziri, manaibu waziri na wabunge wa CCM wanatarajiwa
kuwepo.

0 comments:
Post a Comment