Monday, February 8, 2016

diamond platnumz
Baba mzazi wa msanii wa bongo fleva Diamond Platnumz ameweka wazi hisia zake baada ya kukosa mualiko kwenye arobaini ya mtoto wa Diamond ‘Tiffah’
Baba wa Diamond Platnumz, Abdul Juma amesema hakuna siku alilia kwa uchungu kama siku ambayo mjukuu wake Tiffah alifanyiwa sherehe ya arobaini bila yeye kualikwa
Akizungumza katika kipindi cha Clouds TV Mzee Abdul alidai licha ya kuwa anawasiliana mara kwa mara na mama yake Diamond, lakini hakuwai kupewa taarifa yoyote kuhusu tukio hilo mpaka alivyoona picha kwenye magazeti.
Mzee Abdul alisema “Hakuna kitu kiliniuma kama kufanyiwa shughuli kwa yule dogo bila kualikwa, Yaani nakumbuka nilipigiwa simu nikaambiwa baba mwanao amepata mtoto lakini sio siku ya arobaini, niliumia sana, nililia, nililia sana kutoalikwa kwenye arobaini. Mimi nachoomba (Mama Diamond) asinisahau, kuna kazi nilifanya mpaka akawa hapo 

1 comment:

  1. mzee,achana na kulalamika kwa kila kitu! eh!kuwa karibu na mwanao sasa!kila wakati unamlalamikia matatizo yako kwake kwa watu! endelea kumwombea kwa mwenyezi mungu ampe lililo la heri yeye na familia yake!loh,utamfanya ajute!ndiyo maana tunasisitiza kupanda mbegu nzuri kwa watoto ili hata ukiishiwa nguvu uzeeni akushikilie sasa kina mama wanafaidika sana kwa sababu wanawajali na kuwalea watoto wao katika hali zote za taabu na raha,wakati kinababa walio wengi wanasepa pinedi maugomvi yanatokea!upo mzee! haya msomee dua jema mwanao,mkweo na mjuu wako ni zaidi ya arobaini uliyotaka kuhudhuria

    ReplyDelete