Wednesday, February 17, 2016

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo jipya la Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) leo jijini Dar es Sakaam wakati wa kuzindua jengo hilo na kuwaaga makamishna waliomaliza muda wao. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TACAIDS Bw. Jumanne Isango

mik2
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama akifungua kitambaa kuashiria uzinduzi wa jengo jipya la Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) leo jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua jengo hilo na kuwaaga makamishna waliomaliza muda wao. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TACAIDS Bw. Jumanne Isango na kushoto ni Balozi wa Denmark nchini Bw. Einar Hebogard Jensen.
mik3
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama akifafanua jambo baada ya kupata maelekezo kutoka kwa Mkutubi Bw. Elisha Mngale (kushoto) wakati wa kuzindua jengo jipya la Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) na kuwaaga makamishna waliomaliza muda wao leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TACAIDS Bw. Jumanne Isango na wapili kulia ni Balozi wa Denmark nchini Bw. Einar Hebogard Jensen.
mik4
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TACAIDS Bw. Jumanne Isango akizungumza na makamishna wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi, wakuu wa taasisi za serikali na binafsi pamoja na wadua wa maendeleo wa nchi wahisani (hawapo pichani) wakati wa kuzindua jengo jipya la Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) na kuwaaga makamishna waliomaliza muda wao leo jijini Dar es Salaam.
mik5
Balozi wa Denmark nchini Bw. Einar Hebogard Jensen akitao neno wakati wa kuzindua jengo jipya la Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) na kuwaaga makamishna waliomaliza muda wao leo jijini Dar es Salaam.
mik6
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na makamishna wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi, wakuu wa taasisi za serikali na binafsi pamoja na wadua wa maendeleo wa nchi wahisani (hawapo pichani) wakati wa kuzindua jengo jipya la Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) na kuwaaga makamishna waliomaliza muda wao leo jijini Dar es Salaam.
mik7
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama akimpa cheti cha utendaji kazi mzuri aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji Tume ya Kudhibiti Ukimwi Dr. Fatma Mrisho wakati wa kuzindua jengo jipya la Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) na kuwaaga makamishna waliomaliza muda wao leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Balozi wa Denmark nchini Bw. Einar Hebogard Jensen
mik8
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama akimpa zawadi ya ngao Balozi wa Denmark nchini Bw. Einar Hebogard Jensen kushukuru kwa mchango uliotolewa na nchi ya Denmark kusaidia ujenzi wa jengo la TACAIDS wakati wa kuzindua jengo hilo na kuwaaga makamishna waliomaliza muda wao leo jijini Dar es Salaam.
mik9
: Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama akivaa beji yenye nembo ya kuzuia na kupambana na virusi vya ukimwi kuhamasisha Tanzania isiyokua na virusi vya ukimwi wakati wa kuzindua jengo jipya la Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) na kuwaaga makamishna waliomaliza muda wao leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Balozi wa Denmark nchini Bw. Einar Hebogard Jensen na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TACAIDS Bw. Jumanne Isango.
……………………………………………………………………………………………………………………
Na: Genofeva Matemu – Maelezo
Uboreshaji mipango mikakati ya kupambana na UKIMWI ili kukabiliana na machimbuko ya maambukizi mapya ya UKIMWI nchini imetakiwa kutekelezwa na kila mkoa ikiwa ni lengo la kuzuia maambukizi mapya ya ukimwi, unyanyapaa na vifo vinavyotokana na ukimwi.
Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama wakati wa uzinduzi wa jengo jipya la Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) na kuwaaga Kamishna waliomaliza muda wao leo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mhe. Mhagama amesema kuwa kila mkoa unapaswa kuboresha mpango mkakati wa kupambana na UKIMWI na kuwasilisha taarifa ya utekelezaji kila robo ya mwaka katika ofisi za makao makuu ya Tume ili kuona mwelekeo wa tatizo la ukimwi nchini.
Aidha Mhe. Mhagama ameiomba jamii ya watanzania kuona umuhimu wa kupima virusi vya UKIMWI (VVU) ili kujua afya zao kwani viwango vya maambukizo ya UKIMWI bado vipo juu kwa asilimia 5.1 hivyo ni wajibu wa kila mtu katika jamii kujua afya yake na kuchukua taadhari.
Kwa upande wake Balozi wa Denmark nchini Bw. Einar Hebogard Jensen amesema kuwa nchi ya Denmark imekua ikijitoa kwa kadiri inavyoweza kuhakikisha kuwa mapambano dhidi ya UKIMWI nchini Tanzania yanafanikiwa na kuwa na nchi isiyokuwa na maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi hivyo kujenga jamii yenye afya na uwezo.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Kudhibiti Ukimwi Bw. Jumanne Isango amesema kuwa Tume ipo tayari kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kufikia Tanzania isiyokuwa na Ukimwi, Tanzania isiyokuwa na Unyanyapaa na Tanzania isiyokuwa na maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi.

0 comments:

Post a Comment