Msanii mkongwe wa mziki wa Hip Hop nchini Mwana Fa ameeleza kuwa hana mpango tena wa kuendelea kucheza boxing kwa sababu ya yeye kufanya hivyo anaogopa unaweza kumdhuru.

Mwana Fa ameweka wazi kuwa ni mizuka tu kutoka na kuzungukwa na mchezo huo ukizangatia mtaani kwao huko Tanga watu wengi walikuwa waki cheza huo mchezo.
“Nilitaka kupanda ulingoni kabisa lakini nikaja kufikiria nikaona dah,unaweza ukakalishwa,ukawa unauza magazeti mwaka mzima..sina sababu ya kufanya boxing kama profession…kila mtu mtaani kwetu anapigana ngumi kwa hiyo ilikuwa ni mchezo utakutana nao tu ukikua” alisema Mwana Fa na kuongeza kuwa kwa sasa anafanya kwa kujifurahisha.
Source: Clouds
0 comments:
Post a Comment