Tuesday, February 2, 2016

0128-chris-brown-nia-guzman-tmz-instagram-4
Mama mtoto wa Chris Brown ametoa malalamiko kuwa mtoto wake anaweza kupata madhara kutokana na tabia mbaya ya baba yake ya kuvuta sigara akiwa na mtoto wake.

Nia Guzman ambaye ni mama wa Royalty amesema mtoto wake atapata gonjwa la pumu kutokana na moshi wa tobako wa sigara za baba yake na kwamba Chris amerudia tabia yake ya kunywa sizzurp.
Nia ameomba Chris awe anapimwa kama anatumia dawa zozote za kulevya na ameomba aongezewe pesa za malezi ya mtoto kutoka dola 2500 kwa mwezi mpaka dola 16000.
Chris Brown amekanusha taarifa hizi nakusema yeye na mama yake wanahakikisha mtoto yuko kwenye hali nzuri muda wote na ana afya bora.

0 comments:

Post a Comment