Shamsa Ford.
MSANII wa Filamu Bongo, Shamsa Ford amefunguka kuwa yupo mbioni kutoa filamu mpya inayokwenda kwa jina la Chele Mvuvi aliyowashirikisha wasanii kutoka Tanzania Bara, Haji Adamu ‘Baba Haji’ na wasanii kutoka Zanzibar.
Akizungumza na Championi Jumatano, Shamsa amesema kuwa, filamu hiyo ipo mbioni kutoka mwezi wa tatu akiwa amewashirikisha wasanii wa Bara na Visiwani ili kuweza kuleta ladha tofauti.
“Kwa sasa najiandaa kutoa filamu yangu mpya itakayotoka mwezi wa tatu inayokwenda kwa jina la Chele Mvuvi ambayo imelenga kutoa elimu kwa wavuvi, nitawashirikisha wasanii kutoka Bara na Zanzibar akiwemo Baba Haji.
“Kuhusu kupungua kwa soko la filamu kwa sasa limefifia kidogo lakini si sana hii inatokana na wasanii kulala kwa kutotoa filamu zenye msisimko lakini hali itakaa sawa,” alisema Shamsa.

0 comments:
Post a Comment