Mkali wa Aiyola Harmonize amesema bado anahitaji muda zaidi wa kuendelea kufanya kazi na producer wachanga kwa kuwa ni rahisi kushauria nao.

Akizungumza katika kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM Jumatatu hii wakati akiutambulisha wimbo wake mpya ‘Bado’ ambao amemshirikisha Diamond, Harmonize alisema anapenda kufanya kazi na producer wachanga kwa kuwa wanaweza kushauriana.
“Napenda kufanya kazi na maproduza wadogo, bado nina hali ya uwoga wa kufanya kazi na maproduza wakubwa ambaye ana jina kubwa. Nahisi nitakuwa simtendei haki maana kuna vitu ninavyovipenda viwepo kwenye wimbo wangu pengine yeye akasema visiwepo, nitamsikiliza yeye kwa kumuogopa,” alisema Hamonize
Wimbo mpya wa Hamonize ‘Bado’ umetayarishwa ndani ya Wasafi Studio chini ya producer Lizer Classic huku wimbo wake uliyomtambulisha Aiyola ukiandaliwa ndani studio ya Kazi Kwanza Record chini ya producer Maxmaizer.
0 comments:
Post a Comment