Tuesday, February 23, 2016

Jux - onemorenight-1
Staa wa muziki Jux amedai video ya wimbo wake mpya ‘One More Night’ imekuwa na mafanikio makubwa nje ya nchi kuliko hapa nyumbani.


Akizungumza na Bongo5 Jumamosi hii, Jux alisema amekuwa akipokea comment nyingi nzuri kutoka nje kuhusu video hiyo.
“Video inafanya fresh, inafanya vizuri sana nje kwenye stations kubwa, inapigwa sana. Yaani watu wananiambia kazi ni kubwa na bado naendelea kupata comment nyingi sana kutoka nchi za nje japo kuwa wengi hawaelewi lugha,” alisema Jux
“Pia hata kwa Tanzania kuna baadhi ya mashabiki wangu wanaifurahia sana wanasema nimejaribu kufanya kitu tofauti, sijafanya hivyo before ni kitu kipya, kwahiyo imepokelea vizuri, video na audio vyote vinafanya poa,” aliongeza Jux.
Video ya wimbo One More Night ilitoka December 10, 2015, mpaka sasa imeangaliwa mara 278,269 kupitia mtandao wa Youtube.

CHANZO NA Bongo5.

0 comments:

Post a Comment