Staa wa muziki, Mwasiti amewataka wasanii wa kike wanaoingia kwenye muziki kuwa makini na wanaume wachwara ambao wanadai wanataka kuwasaidia kimuziki kumbe wanataka kuwatumia kimapenzi.
Akizungumza katika kipindi cha Bongo Beats cha Star TV Jumanne hii, Mwasiti alisema wasanii wa kike wanatakiwa kujua wamefata nini kwenye muziki na kuacha kupapatikia mambo makubwa.
“Mimi nafikiri kwanza watoto wa kike wajue wamefata nini kwenye muziki. Hii sanaa ni pana sana na ina watu tofauti tofauti sio unavyowaona wasanii wanakuwa wakubwa ukadhani ni kitu rahisi,” alisema Mwasiti.
“Kwahiyo mabinti wanavyoingia huku sio sehemu nyepesi kama wanavyofikiria kwamba ukiingia huku utapata watu wenye pesa na mabuzi wakukusaidi, watakutumia alafu watakuacha. Kwahiyo mnavyoingia huku mjue nini kimewaleta, vinginevyo wataondoka hata walivyovijia wasivipate,” aliongeza.
0 comments:
Post a Comment