Posted by Williammalecela.com on Tuesday, February 02, 2016
 |
MWILI wa aliyekuwa Mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu wa fani ya Sheria wa
Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB), Calvin Kavishe
unatarajiwa kutolewa
heshima za mwisho Kesho mchana.
Akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi baba wa marehemu,Nicolasi
Kavishe alisema ibada ya kuaga mwili wa marehemu Calvin itafanyika
kuanzia saa Sita mchana Katika Kanisa la Mtakatifu Thomas More lilipo
eneo Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar Es Salaam.
Kavishe alisema
baada ya Misa kumalizika watu watapata fursa ya kutoa heshima za mwili
kwa mwili wa marehemu na Kisha mwili huo kusafirishwa siku hiyo hiyo
kuelekea Rombo Mkuu - Shindi Kati Mkoani Kilimanjaro kwaajili ya Mazishi
yanatarajiwa kufanyika Alhamisi 4/2/2016 saa nane mchana.
Calvin
Ambaye alikuwa akitarajia kuhitimu shahada yake ya sheria Julai maiti
yake imeifadhiwa Katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili alifariki usiku
wa kuamkia Januari 31 Mwaka huu, kwa ajali ya Gari Katika eneo la
Salenda Bridge.
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi 0714 774494 |
0 comments:
Post a Comment