Posted by Williammalecela.com on Wednesday, February 10, 2016
Wachezaji wa timu ya taifa ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamezawadiwa magari ya kifahari baada
ya kushinda Kombe la Taifa Bingwa Afrika kwa wachezaji wa ligi za
nyumbani (CHAN).
Rais Joseph Kabila amemtunuku kila mchezaji gari gari la kifahari aina ya Toyota Prado la thamani ya $60,000 (£40,000). Wachezaji hao pia wamepewa nishani, kwenye hafla iliyoandaliwa ikuluni. "Asanteni sana kwa ushindi huu. Mmewaunganisha Wakongomani wote," alisema Rais Kabila.
Chui hao wa Kinshasa walitwaa kombe kwa kulaza Mali 3-0 kwenye fainali na kuwa taifa la kwanza kushinda kombe hilo mara mbili. Mwaka
2009, mara ya kwanza kuandaliwa kwa michuano hiyo, DR Congo waliondoka
na ubingwa kwa kulaza Black Stars ya Ghana 2-0 kwenye fainali. Image copyrightAFPImage caption
DR Congo walilaza Mali 3-0 kwenye fainali
Mwandishi wa BBC Mbelechi Msochi anasema mchezaji
Heritier Luvumbu Nzinga aliyeumia kwenye michuano hiyo pia ameahidiwa
kwamba atasafirishwa ng'ambo kwa matibabu.
Image caption
Rais Kabila amewapongeza wachezaji wa timu ya taifa
0 comments:
Post a Comment