Wednesday, February 17, 2016




Rapper Nay wa Mitego amesema anafanya nyimbo ambazo zinawafurahisha mashabiki wake.
nay new2
Akizungumza na 255 katika kipindi cha XXL cha Clouds FM Jumatatu hii, Nay alidai mashabiki wake wanapenda nyimbo ambazo anazungumzia wazi wazi bila kuficha.

“Ilishawahi kutokea nilipotoa ngoma yangu ya ‘Salamu Zao’ kuna baadhi ya washikaji zangu ambao nilikuwa nao karibu walinikimbia,” alisema Nay.
“Sijali mtu atanitenga kwa kuwa nimeongea ukweli, ila nitaumia sana kama nikitengwa na mashabiki wangu. Sijawahi kupata vikwazo kama ninavyovipata hivi sasa. Najua kwa wasanii hiki ninachoimba kinaonekana si sawa kwao, ila kwa mashabiki wangu ni sawa,” aliongeza Nay.


0 comments:

Post a Comment