Mtangazaji wa kipindi cha Mkasi ambacho kinarushwa kupitia ting'a namba
moja kwa vijana (EATV) Salama Jabir amefunguka na kuwataka watanzania
kuthamini na kuheshimu watu ambao wanajituma kufanya mambo katika kazi
zao.
Salama amesema kuwa kazi ya msanii siku zote ni sanaa ambayo unaweza kuipenda au kutoipenda.
Salama Jabir amesema hayo kupitia Account yake ya Twitter kufuatia
baadhi ya maoni ya mashabiki ambao wamekuwa wakiwaponda wasanii wa bongo
pindi wanapokuwa wanatoa kazi zao hususani video huku mashabiki wengine
wakienda mbali na kuponda au kuzungumzia jambo kama wao wana maarifa ya
jambo hilo.
"Kazi ya msanii ni Sanaa... Usingiingilie!! ni aidha utaipenda au hutaipenda simple!! Kama rahisi fanya na wewe tuone Respect kwa wanaojituma" Amesema Salama
Imekuwa ni kawaida kwa mashabiki kuponda kazi za wasanii na kuwatusi
kupitia mitandao yao ya kijamii jambo ambalo linakuwa linakatisha tamaa
baadhi ya wasanii na kuwaumiza kwani maneno ambayo mashabiki huwa
wanatumia ni makali na ya kukatisha tamaa.
Hali hii mara nyingi imekuwa ikisababishwa na makundi ya mashabiki
maarufu kama Team, kuna watu wanaweza kuponda jambo ili mradi tu kwa
sababu yeye si shabiki wa msanii fulani na wapo wengine wanafanya hivyo
kwa lengo ya kukomesha, huku wengine wakitaka wasanii waendelee kuleta
video za aina fulani pekee na ukifanya vinginevyo wanaona umekosea kwa
sababu ndicho kitu walichozoea kifupi hawataki kukutana na kitu cha iana
mpya.

0 comments:
Post a Comment