
Kim Kardashian amevumilia vya kutosha tabia ya mume wake Kanye West kuropoka mambo hadharani na sasa huenda akachukua hatua kubwa zaidi.
Kwa mujibu wa jarida la Life & Style, Kim anadaiwa kuwaambia wanasheria wake kuanza kutayarisha talaka ili kama Kanye asipobadilisha mwenendo aachana naye.
Kanye amekuwa akiutumia mtandao wa Twitter kuandika chochote kinachomkera na amejikuta akisema mambo mengi yaliyowashtua wengi. Na sasa Kim anaogopa kuwa vitendo vya mume wake vimeanza kuleta picha mbaya kwake pia.
“Kim amemuomba mume wake kuacha kutweet na apate msaada wa hasira alizonazo na Kanye amemhakikishia mkewe kuwa atabadilika,” chanzo kimoja kililiambia jarida hilo.
Hata hivyo mwakilishi wa Kim amekanusha madai hayo kuwa anataka kuivunja ndoa yake.
CHANZO;BONGO5
0 comments:
Post a Comment