Staa
wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper na mpenzi wake Mkongo, wamedaiwa kuuza
magari yao na kutimkia nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.Chanzo makini kilichoomba hifadhi ya jina, kimepenyeza ubuyu kuwa miezi kadhaa iliyopita, maisha ya Wolper na Mkongo huyo yalibadilika na kuwa magumu hivyo katika kusaka suluhisho la kujikwamua, wakaamua kuuza magari yao na kwenda kuanzisha maisha mapya Sauz.
“Jamani mambo hapa kati hayakuwaendea vizuri Wolper na mpenzi wake hivyo
waliamua kutimkia Sauz lakini waliuza magari yao na kwenda kuendelea na maisha
mengine huko maana Mkongo alikuwa pia na makazi kule,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuinyaka habari hiyo gazeti hili liliwasiliana na Wolper kwa njia ya simu ambapo alikiri kuwa yupo Sauz na mpenzi wake Mkongo lakini akakana vikali suala la wao kuuza magari.
Baada ya kuinyaka habari hiyo gazeti hili liliwasiliana na Wolper kwa njia ya simu ambapo alikiri kuwa yupo Sauz na mpenzi wake Mkongo lakini akakana vikali suala la wao kuuza magari.
“Jamani kwa nini watu wako hivyo mimi sijauza gari langu lolote kama huamini
nenda nyumbani utayakuta watu wanapenda sana kuzungumza vitu ambavyo hawana
uhakika navyo kabisa.
“Tuliamua tu na mpenzi wangu tubadili maisha, tuhamie huku Sauz na si
kwamba maisha Bongo yalikuwa magumu,” alisema Wolper.
Chanzo:GPL
0 comments:
Post a Comment