MUIGIZAJI mkongwe wa filamu Bongo, Blandina Chagula anayefahamika kisanii kama Johari, anadaiwa kuwewesekea penzi la mbunge mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (jina linahifadhiwa) ambaye alifunga ndoa miezi michache iliyopita. Chanzo makini kilicho karibu na
msanii huyo kimeliambia gazeti hili kuwa Johari alikasirishwa na
kushangazwa na hatua ya msanii mwenzake kuolewa na mbunge huyo, ilihali
akijua kuwa yeye aliwahi kuishi naye kimapenzi, ingawa alikataa kuolewa
naye kwa kile alichosema ‘hajatulia’.
“Johari anaweweseka kweli
jamani, yaani kinachomuuma huyo mke wa mheshimiwa ni yeye ndiye
aliyemkutanisha na anajua kila kitu, lakini anashangaa hata ilivyokuwa
hadi akakubali kuolewa naye, yaani ni kama mtu aliyeumia sana,” kilisema
chanzo hicho ambacho kiliomba hifadhi ya jina lake ili kulinda ushoga
wao.
Baada ya kunasa ushahidi unaothibitisha Johari akimzungumzia
mbunge huyo kuonesha anaweweseka, gazeti hili lilimtafuta Johari na
kumwuliza kuhusu tuhuma hizo, lakini msanii huyo aliruka kimanga, akidai
hajawahi kuweweseka kwa penzi la mbunge huyo na wala hajawahi
kuwazungumzia.

0 comments:
Post a Comment