Wednesday, February 10, 2016

@LIVE STRAIGHT TALK:- Matokeo ya Uchaguzi wa Marekani ya awali yanashangaza kidogo ingawa yana ukweli mmoja ambao Dunia nzima inashindwa kuuelewa kwamba Wamarekani ni Wabaguzi wa ajabu sana, Wanampenda Trump kwa sababu ni mbaguzi na wanambagua Mama Clinton kwa sababu ni Mwanamke na hawako tayari kuongozwa na Rais Mwanamke. Kwa Matokeo yaliyokwisha tokea tayari uwezekano wa Mama Clinton kumshinda Mzee Sanders hayapo kabisa ingawa atajaribu sana kupigana huu ulitakiwa kuwa uchaguzi wa bure kwa Mama Clinton, alitakiwa kushinda kwa kishindo kutokana na matayarisho na experience kubwa aliyonayo, lakini Wamarekani ni wabaguzi ndio maana wanampenda sana Trump, ingawa wakilulizwa wanajifanya kukataa kwamba hawamuelewi. Dalili zipo wazi kabisa kwamba Mzee Sanders ataishia kushinda upande wa Democrats, Republican wana tatizo la Mgombea anayefaa Gavana Christie Christie wa New Jersey, alitakiwa kuwa ndiye anayeongoza kwa sababu ya kuwa a good Conservative, lakini Trump mbaguzi ndiye anayekubalika zaidi kwa sasa unless Chama cha Republican kiamue kumchinja kama walivyomfanyia IOWA lakini ameshajua kwamba brass ya chama chake haimtaki kwa hiyo anawatishia kugombea kama Independent kitu ambacho akikifanya ataishia kumsaidia Sanders kushinda uchaguzi wa Rais kirahisi sana. - le Mutuz Nation

0 comments:

Post a Comment