Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi na ukarabati wa barabara za Halmashauri nchini unaotekelezwa kwa ushirikiano na shirika la Maendeleo la Japan ( JICA) mradi unaolenga kuwajengea uwezo wahandisi wa Halmashauri na Mikoa katika kusimamia na kukarabati barabara zilizopo katika maeneo yao kwa kushirikiana na wananchi.
Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Godwin Mpinzile akieleza kwa waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara na ukarabati katika Halmashauri hiyo unaofadhiliwa na JICA ukilenga kuwashirikisha wananchi katika ujenzi na utunzaji wa barabara hizo ili ziweze kudumu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe akimpongeza Mwakilishi Mkazi wa Shirika la maendeleo la Japan (JICA) hapa nchini bw. Nagase Toshio kwa ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Japan hali iliyochangia kufanikiwa miradi ya ujenzi wa barabara katika halmashauri mbalimbali hapa nchini inayofadhiliwa na shirika hilo.
Muwakilishi Mkazi wa Shirika la maendeleo la Japan (JICA) bw. Nagase Toshio akifafanua kuhusu ushirikiano mzuri uliopo kati ya Serikali ya Tanzania na Japan katika kutekeleza mradi huo unaolenga kujenga uwezo kwa wahandisi wa Halmashauri hapa nchini ili waweze kuwashirikisha wananchi katika miradi ya barabara inayotekelezwa ili waweze kujiletea maendeleo .
Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa bw. leopold Runji akitoa ushuhuda wa namna halmashauri hiyo ilivyonufaika na mradi wa ujenzi na ukarabati wa barabara unaotekelezwa katika halmashauri hiyo kwa ufadhili wa shirika la JICA.(Picha zote na frank Mvungi-Maelezo)
………………………………………………………………………………………………………….
Frank Mvungi-MAELEZO
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI bw. Mussa Iyombe amewataka wananchi kutunza barabara zinazojengwa na Serikali kwa kushirikiana na wafadhili katika Halmashauri zote hapa nchini.
Akizungumza leo Jijini Dar es salaam katika hafla fupi ya kupokea ripoti ya utekelezaji wa mradi wa Ujenzi na ukarabati wa barabara za halmashauri nchini Iyombi amebainisha kuwa mradi huo umefadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) .
“Mradi huu unatekelezwa katika Halmashauri za Iringa,Mufindi,Chamwino na Kondoa” alisisitiza Iyombe.
Akifafanunua kuhusu utekelezaji wa mradi huo Iyombe amebainisha kuwa unadhamiria kujenga uwezo kwa wahandisi wa Mikoa na Halmashauri hapa nchini ili waweze kushirikiana na wananchi katika kujenga na kulinda miundo mbinu hiyo kwa maslahi ya Taifa.
Aidha Iyombi amewata wakurugenzi wa Halmashauri ambazo mradi huo unatekelezwa kutunza barabara hizo ili zilete matokeo yaliyokusudiwa.
Akizungumzia ushirikiano mzuri uliopo kati ya Japan na Tanzania Iyombe amesema kuwa maeneo ambayo Tanzania imekuwa ikipata ufadhili kutoka Japan ni Sekta ya Kilimo,Viwanda,Uimarishaji wa Utawala bora.
Kwa upande wake mwakilishi mkazi wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) bw. Nagase Toshio amesema kuwa Shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kutekeleza miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Mradi wa Ujenzi na Ukarabati wa barabara katika Halmashauri hapa nchini unatekelezwa kwa awamu ambapo awamu ya kwanza imekamilika katika Halmashauri za Chamwino na Iringa na awamu ya pili imekamilika katika Halmashauri za Kondoa na Mufindi ambazo ripoti ya utekelezaji wake iliwasilishwa leo katika mkutano wa siku moja ulifanyika Jijini Dar es salaam ukilenga kufanya tathmini ya utekelezaji kabla ya kuanza kwa awamu ya tatu.
0 comments:
Post a Comment