Friday, February 5, 2016

Watu saba wameuwawa kinyama katika kipindi cha miezi miwili maeneo mbalimbali ya jimbo la Muleba kusini mkoani Kagera hali iliyosababisha wananchi kuishi kwa hofu kubwa wakilalamikia vyombo vya usalama kwa kushindwa kuwadhibiti uhalifu.Hayo yamebainishwa na mbunge wa jimbo la Muleba kusini Prof Anna Tibaijuka akiwa na wabunge wa umoja wa katiba UKAWA katika mazishi ya diwani wa kata ya Kimwani kupitia chama cha wananchi CUF Bw.Silvesta Mringa aliyeuwawa kinyama na kusababisha uvunjifu wa amani huku
wananchi wakichukua sheria mikononi kwa kuteketeza kwa moto nyumba nane, gari, mashine za kusaga nafaka na kuhalibu baadhi ya mashamba ya watuhumiwa ambapo jeshi la polisi linawashikilia watu 11 kutokana na matukio hayo.
Kufuatia hali hiyo chama cha wananchi CUF kimelaani vikali mauwaji ya kinyama ya diwani wa kata ya Kimwani Silvesta Mringa huku wabunge wanaounda umoja wa katiba wa UKAWA wakiahidi kutorudi bungeni hadi watakapohakikisha watuhumiwa wa mauaji wote wamekamatwa.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Muleba Bw.Fransice Isack amewataka wananchi kushirikiana na serikali kuwafichua wahalifu waliopo kwenye maeneo yao kwa lengo la kudhibiti uhalifu unaotishia amani katika wilaya ya Muleba.
Marehemu Silvesta Mriga diwani wa kata ya Kimwani aliyeuwawa kinyama ameacha mke na watoto 13 Bwana alitoa na sasa ametwa kwa kuwa amempenda zaidi yetu.

0 comments:

Post a Comment