Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea msaada wa magodoro 120 kwa ajili ya wazazi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Leo. Msaada huo umetolewa na Bohari kuu ya Dawa nchini.
Kutoka Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk UlisubisyaMpoki, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Bohari Kuu ya Dawa, Laurean Bwanakunu akitoa maelezo kabla ya kukabidhi msaada wa magodoro kutoka katika bohari hiyo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akipokea msaada wa magodoro kutoka Bohari Kuu ya Tanzania (MSD).
0 comments:
Post a Comment