Thursday, March 3, 2016


Rapper Ambwene Yessayah aka AY amekutana na maafisa wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA Alhamis hii kwa mazungumzo zaidi.

Mkutano wao umekuja wiki kadhaa baada ya mamlaka hiyo kuifungia video ya wimbo wake Zigo Remix akiwa na Diamond kutopigwa mchana.

AY amepost picha akiwa na Meneja Mawasiliano wa mamlaka hiyo, Innocent Mungi na Naibu Mkurugenzi Masuala ya Watumiaji wa Mawasiliano Thadeo Ringo wakiwa kwenye ofisi za mamlaka hiyo.

Mkutano huo ulikuwa ni kwaajili ya mamlaka hiyo kumwelewesha kwa kina zaidi AY kuhusu sababu za kuchukua uamuzi huo na jinsi ya kushirikiana zaidi ili mambo kama hayo yasitokee tena siku za usoni.

0 comments:

Post a Comment