Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Ally Simba hii leo jijini Dar es salaam na kuongeza kuwa kuna kampuni zilizopewa kibali kusafirisha barua na vifurushi hivyo kama Azam Marine wanataka kufanya shughuli hizo hawana budi kuomba kibali maalum.
Sambamba na kampuni hiyo wameitaka kampuni ya Rifaro Afrika Limited kuacha mara moja kutumia rasilimali namba maalum za TCRA katika kuendelea kutumia huduma za mawasiliano nchini kwani hawana ruhusa ya kuendelea kutumia namba hiyo wakati imeisha muda wake wa matumizi.
TCRA imezitaka kampuni zote zinazotoa huduma za mawasiliano nchini kufuata sheria na taratibu za mamlaka hiyo na kutoa huduma kwa kiwango kilichowekwa na mamlaka kwani kwenda kinyume na taratibu hizo kutapelekea kutozwa faini au hata kunyanganywa kibali cha leseni pale itakapobidi.

0 comments:
Post a Comment