Tuesday, March 1, 2016


Baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda kutangaza kuwa Walimu wa shule za Dar es salaam kuanza kupanda daladala bure baada ya kukubaliana na wamiliki pamoja na madereva wa daladala, watu mbalimbali wamekuwa na  maoni tofauti huku wengi wkimkosoa.

Dc Makonda mwenyewe anasemaje? ‘Najua nipo kwenye jamii ambayo inapenda kuongea sana kuliko kufanya kazi, jamii inayojua kuongelea kukwama kwa jambo hata kabla ya kuanza kufanya kazi ‘

‘Watu wengi wanesema tungewapa pesa ya nauli, wengine wanasema pesa hizi wangepewa wanafunzi, wanasahau kama Walimu ndio uti wa mgongo wa taifa‘

‘Huu ni mchabgo wa wadau, wadau ndio wanawasaidia Walimu, mimi nasimama kama daraja na kufikisha kilio kwa wadau, watu wasichanganye mambo, Mkuu wa Wilaya hana pesa..wao wamepewa usafiri‘

Unaweza kumsikiliza pia Dc Makonda kwenye hii sauti hapa chini….
Categories:

0 comments:

Post a Comment