Monday, March 7, 2016


Issue ya uhaba wa sukari ilichukua headline baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania John Pombe Magufuli kupiga marufuku uingizaji wa sukari kutoka mataifa ya kigeni ili kuvilinda viwanda vya sukari nchini ambavyo vimeathiriwa na uingizaji na uagizaji wa sukari ya bei rahisi kutoka nje. 

Kuzuiwa kwa sukari ya nje ikasemekana kumesababisha tatizo la mfumuko wa bei ya sukari licha ya kuzalishwa kwa wingi hapa nchini. Leo March 7 2016 Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage amezungumzia hilo wakati akijibu maswali ya wanahabari na kukanusha kuwepo kwa uhaba wa sukari nchini….

>>> ‘Hakuna uhaba wa sukari, kuna sukari ya kutosha na ambaye anaficha hiyo sukari yake kwanza nimeshaagiza tena nije nimtafute mkurugenzi wa leseni kama kuna godown lina leseni nikalifunge godown tuone huyo anayeficha sukari‘:-Charles Mwijage

>>>’kwa hiyo hakuna uhaba wa sukari kama kuna mtu anajua kuna mtu anaficha sukari aje aniambie, mimi naweza kufunga godown la mtu yeyote hapa nchini simuogopi mtu yeyote kwa hiyo hakuna uhaba, uhaba unatengenezwa,  mimi nafanya survey nauliza sukari inauzwa bei gani kwenye maeneo mbalimbali nchini‘:-Charles Mwijage

0 comments:

Post a Comment