Tuesday, March 8, 2016

12568246_849512441828114_2017407181_n
 Barakah Da Prince ana ngekewa na watoto wazuri wa mjini. Baada ya Meninah, Linah, Masogange, Nisha na wengine tusiowajua, hitmaker huyo wa ‘Siachani Nawe’ ameangukia kwenye penzi la mtoto wa kihindi, Naj.

Hawajasema na utashangaa tumejuaje. Well wacha tukutoe tongo tongo. Macho ya kidetective yalishtuka baada ya kuona Baraka akipost picha ya Naj Instagram (hiyo chini) na kuandika: Mchizi WANGU rafiki nilie kugundua wa kweli…… God bless u …… @najdattani @najdattani @najdattani.”
12729487_566367356853350_934448113_n
Baada ya muda, Barakah alipost picha Instagram (hiyo chini) kumtambulisha mpenzi wake mpya baada ya kudai kuwa amekuwa akichafuliwa.
Barakah-Da
Barakah aliandika:
My life na huyu tu ndio namtambua, hao mnawatambua ninyi, haya ni maisha yangu,na yapo kwenye serekali yangu, usitake niishi unavyotaka, mnajaribu sana kuchafua jina langu kwa mashabiki zangu, na pia mnajarbu kushusha heshima yangu kwa wanaonieshimu ila mmechelewa sana, nachoamini shabiki wa kweli awezi nichukia kwa upumbavu au uvumi wa kijinga unaoendelea, hii ya mtoto imegoma tengenezi nyingine tena,na tambueni haya ni maisha yangu #SUPER na tumeshamjua anaewatuma kunichafua.
Ni ngumu kutambua sura ya msichana huyo, sasa tumejuaje kuwa msichana huyo ni Naj? Simple. Machale yanaturejesha kwenye kurasa ya Instaram ya Naj na hapo tukatafuta tu kama hivi karibuni alikuwa na msuko kama wa msichana huyo aliyekumbatiwa na Barakah. Na hiyo picha chini ikatupa ukweli:
12729666_840898609389509_1242248601_n
Bado unabisha? Ila Barakah we mbayaaa!!

CHANZO na Bongo5


0 comments:

Post a Comment