Saturday, March 19, 2016

Bob Junior
Msanii na mtayarishaji wa muziki kutoka Sharobaro Record, Bob Junior amenusurika katika tuhuma za kuhusika na ujambazi wa kuteka.

Muimbaji huyo aliingia matatani hivi karibuni baaada ya jeshi la polisi kudai namba yake ya simu ilikuwa ikitumika kuwasiliana na mtu anayedaiwa kutekwa.
“Nashukuru simu imeniokoa maana nilipokamatwa na polisi kituo cha Magomeni kwa tuhuma za ujambazi niliwekwa ndani siku mbili, ndugu zangu walikuja kunidhamini tukaenda kwenye mitandao ya simu, simu yangu ikachunguzwa ikagundulika kwamba sijahusika na suala hilo,” Bob Junior aliliambia gazeti la Mtanzania.
Aliongeza,“Imekua kawaida kwa sisi watu wenye majina makubwa kusingiziwa mambo ili tuonekane tunaishi kwa kuiga, hayo niliyosingiziwa ni chuki tu ambazo hata sijui kwanini zimefanyika hivyo, nami kwa sasa naomba jambo hili liishe ili niwashtaki kwa kunidhalilisha,”

CHANZO na Bongo5.com

0 comments:

Post a Comment