Watangazaji hao, Gerald Hando na Paul James, maarufu kwa jina la PJ,
hawakushiriki kwenye kipindi cha jana asubuhi na Mwananchi ilithibitishiwa baadaye kuwa wamemaliza mikataba yao na uongozi wa kituo hicho hauna mpango wa kuwabakiza.
Dar es Salaam. Watangazaji wawili wa kipindi maarufu cha Power Breakfast kinachorushwa na Clouds FM wameachana na redio hiyo, Mwananchi imetaarifiwa.
Watangazaji
hao, Gerald Hando na Paul James, maarufu kwa jina la PJ, hawakushiriki
kwenye kipindi cha jana asubuhi na Mwananchi ilithibitishiwa baadaye
kuwa wamemaliza mikataba yao na uongozi wa kituo hicho hauna mpango wa
kuwabakiza.
Awali, habari zilienea kuwa wawili hao wamefukuzwa
kazi kutokana na matatizo ya kinidhamu. Lakini alipoulizwa kuhusu suala
hilo, Hando alijibu: “Sijafukuzwa kazi hata kidogo, wala sijaacha kazi.
Ninachofahamu mimi ni mfanyakazi wa Clouds Redio na leo (jana)
sikusikika kwenye kipindi kwa sababu nilikuwa na udhuru.”
Uongozi wa Clouds unatarajia kutoa taarifa rasmi leo asubuhi kwenye kipindi cha Power Breakfast.
0 comments:
Post a Comment