Posted by Williammalecela.com on Thursday, March 17, 2016
Mapokezi na makabidhiano ya Mkuu Mpya wa Mkoa wa Mbeya Anos Makalla na Mkuu mstaafu Mkoa wa Mbeya mhe Abas Kandoro Mkuu wa Mkoa Mbeya ametoa maagizo yafuatayo
1. Watumishi wa umma wafanye kazi kwa bidii washughuliie Kero za
wananchi kwa haraka na ameagiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi kila siku
ya Alhamis ya wiki kuanzia saa 4.00 asub mpaka saa nane ni siku ya
kusikiliza Kero za wananchi na kuzipatia majawabu 2. Ugonjwa wa kipindupindu utokomezwe hataki kusikia ugonjwa wa kipindupindu unaendelea kuwepo mkoani humo
3. Upungufu wa madawati ameagiza kutumia Fedha za halmashauri hasa
mapato ya ndani na wadau msamiati wa upungufu wa madawati uishe mwisho
mei 31 mwaka huu 4. Watumishi hewa Ameagiza maafisa utumishi
kuwajibika ndani ya siku 12 wawabaini na kuondoa watumishi hewa na
kwamba ikifika mwisho wa mwezi wakagundulika watumishi hewa wakurugenzi
na maafisa utumishi watapoteza kazi 5. Michezo amefurahi kuletwa
Mkoa wenye timu mbili zilizo ktk ligi kuu kama mdau wa michezo amewataka
wadau wa Michezo kushirikiana kwa pamoja kuzipatia ushirikiano timu za
prisons na Mbeya city zizidi kufanya vizuri ligi kuu
0 comments:
Post a Comment