#Repost @cloudstv with @repostapp
・・・
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli na
Mkewe Mama Janeth Magufuli leo asubuhi wamepiga simu moja kwa moja
katika kipindi cha #Clouds360
na kuwapongeza Watangazaji hao kwa kazi nzuri wanayoifanya. Mh Rais
alisema kuwa yeye ni shabiki namba moja wa kipindi hicho na
anafurahishwa na kazi nzuri inayofanywa na #CloudsMediaGroup kama zoezi zima la #MalkiaWaNguvu na mengine mengi. Wakimalizia kuonge na watangazaji wa #Clouds360
waliwataka nao wakati mwingine waje na wenzi wao katika kipindi sio
kila mara waje wenyewe 😂. Tunamshukuru Mh. Rais kwa kitendo chake
hichi, hili linaonyesha kuwa tunaifanya kazi vizuri lakini pia ni faraja
kwetu kwani tunaamini sisi ndio kituo cha kwanza Mh. Rais kufanya
kitendo hiki. Mungu Ibariki Tanzania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


0 comments:
Post a Comment