Bendi ya muziki QS International Band inatarajia kumsign msanii Bushoke ili ashirikiane na Q Chief katika kuandaa muziki pamoja na kuipeleka bendi hiyo mbali zaidi.
Akizungumza na Bongo5 Alhamisi hii, Q Chief amesema tayari mmiliki wa bendi hiyo, QS Mhonda yupo kwenye mazungumzo ya mwisho na staa huyo wa wimbo ‘Dunia Njia’.
“Sasa hivi kusema kweli bendi inaelenda vizuri na bado tunaelea kuiboresha zaidi kwa kumwongeza Bushoke ndani ya Bendi,” alisema Q Chief.
“Unajua mimi namkubali sana Bushoke, kwa hiyo hata kufanya nae kazi ni sehemu ya mafanikio yangu pamoja naya bendi. Kwa hiyo tuombe mungu mambo yaende poa hivi karibuni atatambulisha ndani ya Escape One,” aliongeza Q Chief.

0 comments:
Post a Comment