Monday, March 14, 2016


Kuelekea uchaguzi mkuu wa marudio Zanzibar chama cha upinzani cha CUF ambacho kimetangaza kutoshiriki uchaguzi huo  kimevisihi vyombo vya  ulinzi na usalama kusimamia amani  kwa sheria na katiba  ili kunusuru  wakimbizi wa siasa kutokana na hofu kubwa iliyotanda kisiwani pemba  ambapo baadhi ya watu wako Mafichoni.


Msimamo huo umetolewa na kaimu mkurugenzi  wa habari,ueneiz na  mawasilaino kwa Umma Bw.Hamad Masoud wakti akiongea na wandishi wa habari ambapo amesemea hali kiswani Pemba sasa si shwari huku wanchi wakinyimwa fursa zao za haki za binaadamu  ambapo hivi sasa watu hawaruhusiwi kuwepo mitaani ikifika saa mbili usiku na baadhi ya watu wamekimbia makazi yao.

Aidha chama hicho  kimevisihi vyombo vya ulinzi na usalama kuacha kuegemea upande mmoja na kutekeleza wajibu wao kwa misingi ya sheria na katiba huku chama hicho kikishtushwa na ujio  na uingwizaji mkubwa wa askari  na magari na zana nzito za kivita hivyo CUF imetaka amani  isimamaiwe kwa wote.

Kukiwa kumebakia siku sita kufanyika uchaguzi huo wa machi 20 kwa upande wa unguja hali ianendelea kuwa shwari na wanachi kuendelea na shugulki zao kama akwaida huku mazungumzo makubwa ya mitaa mbali mbali na suala la uchaguzi huo wa jumapili.

0 comments:

Post a Comment