Diamond Platnumz amesema wasanii wengi wa Tanzania na Afrika Mashariki kiujumla wanapotea kwenye ramani ya muziki kwasababu wanaendekeza mashauzi, starehe na kutaka kujionesha.
Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, Diamond alisema:
“Unajua wasanii wengi wanapoteza na kushuka kimuziki sababu ya starehe pamoja na mashauzi. Unakuta mtu amepata mafanikio kidogo anaanza mashauzi na kufanya starehe zisizo na tija, ndiyo maana mimi huwezi kuniona kwenye starehe hata wasanii wa WCB ni hivyo hivyo.”
Katika hatua nyingine Diamond alimwelezea Shettah na kusema ni mfano mzuri.
“Mimi namkubali sana Shettah kwani jamaa ni bahili sana anaweza kutoka kufanya show na akakwambia sina pesa, hata gari yake aliyonunua juzi amenunua kwa pesa zake sababu anakusanya pesa zake na kufanyia vitu vya msingi. Sasa hivi Shettah anajenga nyumba yake na hiyo yote sababu si mtu wa mashauzi na wala si mtu wa starehe.”

0 comments:
Post a Comment