Wednesday, March 2, 2016

MPA1
WAZIRI wa Fedha na Mipango , Dakta Philipo Mpango, amesisitiza wafanyabiashara kuhakikisha wanalipa kodi zao kwa wakati  na kuwaonya wale wote ambao watakwepa  watashughulikiwa kwa mjibu wa sheria ili kuboresha huduma za jamii na maendeleo ya taifa.
Alisema kuwa serikali  mkakati wa serikali ni  ni kuongeza makusanyo na kulinda utulivu wa uchumi ukuaji wake kwa kasi zaidi  kwa kuwa wafanyabiashara ndio injini ya chumi wa taifa.
Alisema nchi yetu ina utajiri mkubwa wa raslimali ila bado nchi ni masikini  akasisitiza umuhimu wa kila mmoja kulipa kodi na kuwahakikishia kuwa  serikali  haitamuonea mfanyabiashara yeyoyte  na badala yake kutajengwa mazingira ya kuwawezesha kulipa kodi bila usumbufu.
Ametumia fursa hiyo kuwaonya wafanyabiashara ambao wanashirikiana na baadhi ya wafanyakazi wa mamlaka ya mapato TRA, ambao sio waadilifu kukwepa kodi watatumbuliwa majipu
Alisema serikali itanunua mashine za EFD na kuzigawa kwa wafanyabiashara wote bure lengo ni kuhakikishia zinatumika katika manunuzi na mauzo ya bidhaa kwa ajili ya kutolea risti kwa mununuzi.
Amesema lengo la kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu  wa kulipa kodi ili kujenga Tanzania mpya yenye  uchumi wa viwanda,na hiyo ndio vipaumbele vya mwaka wa fedha  2016/17.
Alisema atafuta kodi zote ambazo ni kero na tayari wizara imeshaziandikia wizara zingine na halmashauri  kuainisha kodi zenye kero ili zifutwe kwenye bajeti ijayo.
Wakichangia kwenye kikao hicho wafanyabiashara wameihakikishia serikali kuwa watalipa kodi ila wanataka kushirikishwa kwenye utungaji wa sera .
Awali mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda,amesema mkoa wa Arusha unakumbana na changamoto mbalimbali zikiwemo za sekta ya madini  kuwa na makusanyo kidobo kutokana na madini kutoroshwa kwa kupitia mpakani kutokana na eneo la mpaka kuwa kubwa mno.
Waziri alikuwa akizungumza na wafanyabiashara wa mkoa wa Arusha ili kuwasikiliza kero zao ambazo zinasababisha kodi kutokulipwa ipasavyo na hivyo kuikosesha serikali mapato.

0 comments:

Post a Comment