Wednesday, March 16, 2016

Marekani
Mgombea urais wa Marekani, Marco Rubio Jumanne hii ametangaza kujiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho baada ya Donald Trump kushinda kwenye jimbo lake mwenyewe (Rubio) la Florida.

Kujitoa kwa Rubio kunawaacha wagombe watatu wa chama cha Republican, Trump anayeongoza, akifuatiwa na Ted Cruz na John Kasich.
CNN inatabiri kuwa Kasich, 63, atashinda kwenye jimbo lake la Ohio, wakati Trump akitabiriwa kushinda huko North Carolina, huku matokeo yakiendelea kuhesabiwa kwenye majimbo ya Illinois na Missouri.
Tajiri huyo mwenye miaka 69 pia alishinda huko Northern Mariana Islands.
Kwa upande wa chama cha Democratic, Hillary Clinton alimshinda Senator Bernie Sanders jimboni Florida. Clinton pia anatabiriwa kushinda kwenye majimbo ya North Carolina na Ohio, huku matokeo kwenye majimbo ya Illinois na Missouri yakiwa bado.

CHANZO na Bongo5



0 comments:

Post a Comment