Waliofariki katika ajali ni Hilda Msele (59), Mkuu wa Idara ya Mipango ya Uchumi, Makame Ally (40), Dereva wa Tasaf, Khalid Hassan (40), Tunsime Duncan, Mwanasheria wa Wilaya, Juliana Msaghaa, Mhandisi wa Maji wilaya na Ludovick Palangya, Mchumi.
Majeruhi waliolazwa katika hospitali ya Taifa ua Muhimbili ni Ibrahim
Matovu, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Bagamoyo, Dorothy Njetile,
Mratibu wa Tasaf, George Mashauri, Mweka Hazina wa Wilaya, Amadeus
Mbuta, Mshauri wa Tasaf, Julius Mwanganda, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya
Jamii, Tauliza Halidi, Mwananchi na Amari Mohamed, Mwananchi.
Aliyepelekwa katika hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo na kuruhusiwa ni
George Mbilinyi ambaye ni Afisa Utumishi na Utawala wa Wilaya.
Ajari hiyo iliyohusisha lori la mchanga, gari dogo yaliyokuwa yanatokea
Bagamoyo kuja Dar es Salaam, na magari mawili yaliyokuwa kwenye msafara
wa Kamati hiyo, yaliyokuwa yanaenda Bagamoyo kwa shughuli zake za
kibunge.
Magari yaliyokuwa katika msafara wa kamati hiyo, ni gari la Mfuko wa Maendeleo
ya Jamii (Tasaf) na gari la Mkurugenzi wa Wilaya ya Bagamoyo ambayo
yaligongwa na lori hilo la mchanga na kusababisha vifo vya watu hao na
kuwajeruhi wengine kadhaa.
Ajali hiyo ilitokea baada ya gari dogo lililokuwa linatokea Bagamoyo
kupunguza mwendo ghafla na kusababishwa lori lililokuwa nyuma yake
kuligonga na kuhama upande wa pili na kuyagonga magari mawili yaliyokuwa
katika msafara wa kamati ya Bunge.
0 comments:
Post a Comment